About Sahara T.A.G

Hapa Sahara tunaamini  ...

 1. ... kwamba Maandiko Matakatifu yamevuviwa na Mungu na ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu.
 2. ...kwamba Kuna Mungu wa kweli mmoja tu-aliyejidhihirisha katika nafsi tatu...Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu (ambao hujulikana zaidi kama Utatu)
 3. ... kuhusu Uungu wa Bwana Yesu Kristo. Kama Mwana wa Mungu,Yesu alikuwa na Uanadamu na Uungu.
 4. ...kwamba Ingawa alikuwa mwadilifu mwanzoni, mwanadamu alianguka kwa hiari yake ya kutotii akawa chini ya adhabu ya kifo, siyo tu cha mwili bali pia cha kiroho.
 5. ...kwamba Kila mtu anaweza kurudisha ushirika na Mungu kwa 'Kuokoka' (kuupokea msamaha wa dhambi wa Kristo).
 6. ...na kuzitimiza kanuni mbili - (1)Ubatizo wa Maji kwa kuzamishwa baada ya kutubu dhambi na kuipokea zawadi ya Kristo ya Wokovu, na (2) Ushirika Mtakatifu (Chakula cha Bwana) kama kumbukumbu ya kuteswa na kufa kwake kwa ajili ya wokovu wetu.
 7. ...kwamba Ubatizo kwa Roho Mtakatifu hufuatia kuzaliwa upya ambao huwapa waumini nguvu za ushuhudiaji na utumishi, kama ilivyokuwa nyakati za Agano jipya.
 8. ...kwamba Ushahidi wa Ubatizo kwa Roho Mtakatifu ni 'Kunena Kwa Lugha,' kama ilivyotokea Siku ya Pentekoste na kuripotia katika Matendo ya Mitume na Nyaraka.
 9. ...kwamba Utakaso Hufanyika kwa mara ya kwanza wakati wa Kuokoka na siyo tu ni tangazo kuwa mwamini ni mtakatifu, bali pia ni mchakato endelevu kwa kujitenga na uovu wakati mwamini anapozidi kumkaribia Mungu na kufanana zaidi na Yesu.
 10. ...kwamba Kanisa Lina Huduma Yake ambayo ni kuwatafuta na kuwaokoa wote waliopotea dhambini.Tunaamini kuwa 'Kanisa' ni Mwili wa Kristo na linajumuisha watu wote ambao walioupokea ukombozi utokao kwa Mungu (Bila kujali dhehebu) kwa njia ya kifo cha dhabihu cha Mwana Wake Yesu Kristo.
 11. ...kuhusu Viongozi Walioitwa na Mungu, wakasimikwa ki-maandiko, ili walihudumie Kanisa. Biblia inatufundisha kuwa kila mmoja wetu ambaye ni kiongozi lazima aazimie kuwaleta wengine kwa Yesu, kumuabudu Yeye akijumuika na waamini wengine, na kuujenga mwili wa waamini-Kanisa.
 12. ...kwamba Uponyaji wa Kiungu Upo Kwa ajili ya Wakristo wa Sasa na hupatikana kwa njia ya Kifo chake Yesu cha dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu.
 13. ...kuhusu Tumaini Lenye Baraka - Wakati Yesu Atalinyakua Kanisa Lake Kabla ya Kurudi Duniani (Kuja Mara ya Pili). Wakati huo utakapofika, Waamini wote waliokufa katika Kristo watafufuliwa na kunyakuliwa kwenda kukutana na Kristo Yesu mawinguni. Wakristo walio hai Watanyakuliwa pamoja nao kwenda kuishi na Bwana milele.
 14. ...kuhusu Utawala wa Kristo wa Miaka Elfu wakati Yesu atakaporudi pamoja na watakatifu wake wakati wa Kuja Kwake Mara ya Pili Na kuanza utawala wake duniani wa muda wa miaka elfu. Utawala wa miaka elfu utaleta wokovu wa taifa la Israel na amani duniani kote.
 15. ...kwamba Hukumu ya Mwisho Itafanyika kwa wale waliomkataa Kristo. Watahukumiwa kwa dhambi zao kwa kutupwa katika ziwa la moto kwa adhabu ya milele
 16. ...na tunatazamia Mbingu Mpya na Dunia Mpya ambayo Kristo aliiandaa kwa watu wote waliompokea. Tutaishi naye milele baada ya utawala Wake wa Miaka Elfu. 'Na tutakuwa na Bwana milele'